ZIARA YA DKT SAMIA INDONESIA YAMNUFAISHA BEATRICE

 

ZIARA YA DKT SAMIA INDONESIA YAMNUFAISHA BEATRICE

ZIARA YA DKT SAMIA INDONESIA YAMNUFAISHA BEATRICE 

DAR ES SALAAM.

Ziara ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan nchini Indonesia imeleta furaha na matumaini mapya kwa mjasiriamali Beatrice edward mwalingo (Mtandao wa instagram anatumia jina la Beatrice_only1) hii ni baada ya kujibiwa ujumbe na Mhe Rais kuhusu ombi lake la kubebewa cherehani pindi Dkt Samia atakarudi nchini kutokea Indonesia.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan januari 24 aliandika “Nimewasili nchini Indonesia kwa Ziara ya Kitaifa ya siku 3, kufuatia mwaliko wa kaka yangu, Mheshimiwa Rais @jokowi. Uhusiano wa Tanzania na Indonesia ambao mapema mwezi huu (Januari 13) ulitimiza miaka 59, umekuwa wenye tija kwa nchi yetu na mamilioni ya Watanzania hasa kwenye kilimo na biashara. Tunaendelea kuifanya kazi ya kukuza uhusiano huu ili kuleta tija zaidi kiuchumi kwa nchi yetu”

Baada ya chapisho hilo la Mhe Rais Dkt Samia kupitia uwanja wa wachangiaji (comments) Beatrice aliandika ujumbe uliosomeka “Sawa mama. Ukiwa unarudi nyumbani naomba uniletee zawadi ya Cherehani.”

Kufuatia ujumbe huo wa Beatrice Dkt Samia amejibu “Hujambo, Beatrice? Nimepata wasaa wa kuusoma ujumbe wako. Hongera kwa kazi na kujituma. Wasaidizi wangu watawasiliana na wewe kukusaidia upate mashine uliyoomba kwa shughuli zako. Nakutakia kila la kheri”

DKT SAMIA NI RAIS WA WOTE.