BIASHARA KATI YA TZ NA INDONESIA MWAKA 2022 ZILIFIKIA TSH BIL 238
INDONESIA
Ikiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan anaendelea na ziara ya kiserikali ya siku tatu nchini Indonesia kuanzia Januari 24 hadi 26, 2024 tunakukumbusha manufaa yaliyopatikana kutokana na uhusiano thabiti uliopo baina ya nchi hizi mbili.
Takwimu zinaonesha kuwa jumla ya biashara kati ya nchi hizi mwaka 2022 zilifikia shilingi bilioni 238.
Pia Mwaka 2022, mauzo ya Tanzania kwenda Indonesia yalikuwa takriban shilingi bilioni 65 ikilinganishwa na shilingi bilioni 43 mwaka 2021.
Ziara ya Kiserikali ya Rais Samia inatarajiwa sio tu kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Indonesia lakini pia kufungua njia mpya za ukuaji wa uchumi na ushirikiano katika sekta mbalimbali.
#BIMKUBWAINDONESIA