UKUAJI WA UCHIMI TANZANIA WAWAKOSHA WACHUMI
DAR ES SALAAM
Wataalamu wa uchumi kutoka maeneo tofauti nchini wamekoshwa na ukuaji wa uchumi uliopo kwa sasa Tanzania na unaotarajiwa hii ni kutokana na kuimarisha hali ya kujitegemea katika maeneo muhimu ya kimkakati kama vile nishati na uzalishaji wa kilimo hatua ambazo zitapunguza mno athari za mvutano wa kijiografia, kama vile vita vya Urusi na Ukraine, katika uchumi.
Chanzo: Mahojiano kupitia Ripoti ya Hali ya Uchumi Duniani na Matarajio ya 2024 iliyotolewa hivi karibuni.
Ripoti hiyo inakadiria kuwa ukuaji wa uchumi barani Afrika utaendelea kuongezeka kutoka wastani wa 3.3% mwaka 2023 hadi 3.5% mwaka 2024.Ripoti ya Hali ya Kiuchumi na Matarajio ya Dunia 2024 imetolewa na Idara ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (UN DESA), kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) na tume tano za kanda za Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na Uchumi. Tume ya Afrika (ECA), Tume ya Kiuchumi ya Ulaya (UNECE), na Tume ya Kiuchumi na Kijamii ya Asia Magharibi (ESCWA).
KUMBUKA:-Mwaka 2023, Pato la Taifa la Tanzania (GDP) lilikua kwa 5.2% na linatarajiwa kufikia 5.8% Mwaka 2024.