“TUENDELEE KUWA WAMOJA”DKT SAMIA

 

“TUENDELEE KUWA WAMOJA”DKT SAMIA

“TUENDELEE KUWA WAMOJA”DKT SAMIA

DAR ES SALAAM,

Rais wa Jamhri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaasa watanzania kudumisha umoja na mshikamano ili kujenga taifa lenye nguvu na ushirikaino zaidi.

Dkt Samia ametoa wito huo Januari 21, 2024 wakati akizungumza kwenye ibada maalumu ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Dkt. Alex Gehaz Malasusa iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Azania Front Jijini Dar es Salaam na kuhuduhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini serikali pamoja na waumini wa dini ya kikristo kutoka ndani na nje ya nchi.

Mhe. Samia amesema “Tukiwa wamoja tutajenga taifa lenye umoja na mshikamano,na lenye watu wanaoheshiamiana na kuthaminiana,ili tuweze kupiga hatua kubwa za kimaendeleo ni lazima tuendelee kuwa wamoja kwa kuhubiri na kuishi kwa umoja”

Aidha Mhe Rais Dkt Samia kueleka uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu  amevitaka vyama vya siasa kuteua wagombea wazuri ili wananchi waweze kuchagua viongozi wanaowafaa.