TSH BIL 48 ZAWAPA NEEMA WANAFUNZI WA STASHAHADA
MBEYA
Serikali ya awamu ya sita imetenga jumla ya shilingi bilioni 48 kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa stashahada kwa mwaka wa masomo 2023/2024
Chanzo:- Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye uzinduzi wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Mbeya (CUoM) Mkoani Mbeya.
Mpango huo ambao ni dira na maagizo ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan unaolenga kuhakikisha utoaji wa elimu bora utakaowawezesha wahitimu nchini kujiamini na kuhimili ushindani katika soko la ajira kitaifa na kimataifa, pia Dkt Samia analenga kuona vijana wengi wanapata elimu ambayo inawapa ujuzi na uwezo wa kushiriki katika ujenzi wa taifa.