TSH MIL 869.5 ZAJNEGA NA KUKRABATI HOSPITALI MPANDA.
KATAVI
Serikali ya awamu ya sita imetoa kiasi cha shilingi milioni 869.5 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati na ujenzi wa majengo mapya katika Hospitali ya manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.
Mradi huo umejumuisha ukarabati wa majengo 9 na ujenzi wa majengo mapya manne huku jengo moja likimaliziwa na ukarabati huo umekamilika Oktoba 2023 huku lengo likiwa ni kuboresha huduma kwa wakazi wa manispaa ya Mpanda.