TSH BIL 755 ZATEKELEZA MIRADI KILIMANJARO
KILIMANJARO
Serikali imetoa zaidi ya Sh bilioni 755 katika kipindi cha miaka miwili na nusu fedha zilizotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo Kilimanjaro.
Fedha hizo zimetumika kwenye ujenzi wa jengo la mionzi Hospital ya KCMC, kuboresha huduma ya afya pia jengo la mama na mtoto katika hospitali ya Mawezi pia manunuzi ya vifaa tiba,mradi mkubwa wa maji Same, Mwanga -Korogwe,na Hospitali kubwa ya Wilaya ya Same huku lengo la Mhe.Rais Dkt Samia likiwa ni kuona Wananchi wake wananufaika na huduma pia kupiga hatua kimaendeleo