KM 612.14 ZA BARABARA KUJENGWA MOROGORO
MOROGORO
Serikali imeidhinisha fedha kwa ajili ujenzi wa barabara mpya zenye urefu wa kilometa 612.14 kwa kiwango cha lami mkoani Morogoro huku miradi hiyo ikitarajiwa kuufungua mkoa huo kwa kuunganisha halmashauri zake zote.
Miradi hiyo ya ujenzi wa barabara ya ni pamoja na Ubena Zomozi - Ngerengere (Km 11.6), barabara ya Ifakara - Mbingu (km 62.5), barabara ya Mbingu - Chita JKT (km 37.5), barabara ya Ifakara - Lupiro - Mahenge/ Lupiro - Malinyi- Kilosa kwa Mpepo- Londo - Lumecha na Malinyi JCT - Malinyi (km 422.54) na barabara ya Bigwa - Mvuha (km 78) pamoja na madaraja ya Ruvu na Mvuha.
Barabara hizi zote zikikamilika zitainua uchumi wa wananchi wa mkoa wa Morogoro pamoja na kuchochea maendeleo yake maana ni barabara za kimkakati.