TSH BIL 6.7 KWENYE MIRADI YA MAENDELEO
SHINYANGA
Jumla ya Shilingi Bilioni 6.7 (6,705,107, 554. 34) zimetolewa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kutekeleza zaidi ya miradi 19 ya maendeleo katika Manispaa ya Shinyanga mjini kwa Mwaka wa fedha 2022/2023.
Fedha hizo ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na shughuli zingine katika sekta ya elimu, afya,utawala na mfuko wa kuchochea maendeleo.