TSH BIL 52 KUJENGA SKIMU YA MKOMBOZI
IRINGA
Kiasi cha shilingi bilioni 52 kimetolewa na serikali ya awamu ya sita kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa skimu ya Mkombozi iliyopo katika kata ya Mboliboli kata ya Itunundu katika tarafa ya Pawaga,Halmashauri ya wilaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa.
Mradi huo unatarajiwa kukamilika February 2024, ambapo una jumla ya hekta 6000 na kukamilika kwake kutaleta tija kwa wakulima,pia sekta ya umwagiliaji kufikia malengo ya agenda 1030.