BAJETI YA NIRC NI TSH BIL 373
DODOMA
Serikali kupitia wizara ya kilimo imetenga kiasi cha shilingi bilioni 373 bajeti ya mwaka 2023-2024 kwa tume ya Taifa ya umwagiliaji kwa ajili ya kumalizia miradi inayoendelea kujengwa, miradi 25 mipya, miradi 30 ya ukarabati na miradi 42 ya Usanifu.
Aidha kupitia bajeti ya 2023-2024 Tume ya Taifa ya Umwagiliaji itawekeza Kwa wakulima wadogo wadogo Kwa kuchimba zaidi ya visima 1,845 katika Halmashauri zote 184 ambapo wakulima 150 Kila Halmashauri watafungiwa mfumo wa Umwagiliaji ili Kila Mkulima aweze kuzalisha kwenye hekari zake mbili na nusu Kwa lengo la kuongeza tija ya Kilimo Cha Umwagiliaji miongoni mwa jamii.
Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inahamasisha sekta binafsi Kilimo Cha mashamba makubwa (Block Farm) kwaajili ya vijana na akina mama katika mikoa ya Kigoma, Njombe, Mbeya, Kagera na Dodoma kupitia programu ya Build Better Tomorrow (BBT)