TANZANIA NAFASI YA PILI UZALISHAJI TUMBAKU 2022/2023

TANZANIA NAFASI YA PILI UZALISHAJI TUMBAKU 2022/2023

 DODOMA 

Tanzania ni nchi ya pili barani Afrika kwa uzalishaji wa tumbaku kwa mwaka 2022/2023 ambapo uzalishaji nchini umeongezeka kutoka tani 50,000 hadi tani 122,858 mwaka 2022/2023 na matarajio ni kufikia tani 200,00 kwa msimu wa 2024/2025 na tani 300,000 ifikapo 2025/26.Chanzo:- Wizara ya kilimo

Ripoti kutoka wizara ya kilimo inasema  Zimbabwe inaongoza kwa kuzalisha tani 296,000, ikifuatiwa na Tanzania 122,858, Malawi (tani 121,000), Msumbiji (tani 65,800), Zambia (tani 44,000) na Uganda (tani 13,000) Hadi kufikia Desemba mwaka jana, thamani ya mauzo ya tumbaku ilikuwa ni zaidi ya shilingi bilion 791 huku lengo likiwa ni kufikia shilling trilion 1.