REPOA WAIPONGEZA SERIKALI MAGEUZI SERA YA KODI SEKTA YA FEDHA

REPOA WAIPONGEZA SERIKALI MAGEUZI SERA YA KODI SEKTA YA FEDHA

 DAR ES SALAAM 

Wachambuzi wa uchumi na fedha wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa mageuzi ya sera ya kodi na sekta ya fedha hali iliyoitoa kimasomaso sekta binafsi.Wamesema kuimarika kwa sekta binafsi kunatoa mwanya kwasekta ya ajira kuimarika kwa kuwa sekta binafsi ndio kichocheo na uti wa mgongo wa upatikanaji wa ajira Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti (REPOA), Dk Donald Mmari ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya uchumi amesema mabadiliko ya sera ya kodi ambayo ni utashi binafsi wa Rais Samia Suluhu Hassanyamesababisha kufanyika kwa makadirio sahihi ya kodi bila kumwonea mtu hali ambayo imeamsha ari ya biashara na uwekezaji nchini.

Nae Profesa Humphey Moshi Mchambuzi wa masuala ya uchumi, amesema sekta binafsi imeimarika katika mikopo kutokana na mageuzi ya sekta ya fedha yaliyofanywa na serikali ambapo madeni chechefu yalipungua na kutoa mwanya kwa wakopaji kuchukua mikopo.

REPOA waipongeza serikali ya Samia