TSH BIL 49 KUIMARISHA UTOAJI WA HAKI NCHINI

TSH BIL 49 KUIMARISHA UTOAJI WA HAKI NCHINI

DAR ES SALAAM

Novemba  2023 Mahakama ya Tanzania ilisaini mikataba yenye thamani ya shilingi Bilioni 49 na makampuni manne kwa ajili ya ujenzi wa Vituo Jumuishi vya Haki (IJCs) sita katika mikoa ya Songea, Katavi, Geita, Njombe, Simiyu na Songwe lengo likiwa ni kuboresha miundombinu ya mahakama ili ziharakishe utoaji haki kwa wananchi.

Ujenzi wa Vituo hivyo utafanya jumla ya vituo vya Haki Jumuishi vya Tanzania kufikia 12. Hivi sasa, kuna vituo sita vinavyotoa huduma za kimahakama katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Arusha na Morogoro.Utekelezaji wa ujenzi wa majengo ya vituo hivyo jumuishi unafanyika ndani ya miezi tisa na inatakiwa kujengwa katika ubora unaotakiwa