TANZANIA KITOVU CHA UCHENJUAJI MADINI AFRIKA
SAUDI ARABIATanzania imedhamiria kuwa kitovu cha uchenjuaji na uongezaji thamani madini kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.Lengo ni kuongeza fursa za ajira na mapato kutokana na mnyororo wa thamani kwenye sekta ya madini.
CHANZO:- Wizara Ya Madini kupitia mkutano mkubwa wa madini wenye madhumuni ya kujadili nafasi ya madini katika maendeleo ya nchi wazalishaji wa madini uliofanyika Jijini Riyadh, Saud Arabia.
Hatua ambazo serikali inaendelea kuchukua kupitia mapitio ya sera na sheria juu ya kuweka msisitizo kwenye uongezwaji wa thamani ya madini yanayozalishwa nchini.
KUMBUKA :- Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa kinara wa kusimamia uongezaji thamani madini ili kutoa fursa kwa watanzania wengi zaidi kunufaika kupitia mnyororo wa thamani wa madini.
