DKT SAMIA AWATAKIA HERI TAIFA STARS

DKT SAMIA AWATAKIA HERI TAIFA STARS

ZANZIBAR 

Mh Rais Dkt  Samia Suluhu Hassan amezungumza na wachezaji wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu (Taifa Stars) jioni hii kwa njia ya simu na kuwapa moyo kuelekea mchezo wao wa leo na timu ya Taifa ya Morocco ikiwa ni mechi yao ya kwanza katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON2023 yanayofanyika nchini Ivory Coast.Dkt Samia amezungumza na timu hiyo ya Taifa akiwa visiwani Zanzibar tarehe 17 Januari, 2024.

KILA LA KHERI TAIFA STARS