TANZANIA YAPEPEA UTEKELEZAJI AGENDA YA 2063

TANZANIA YAPEPEA UTEKELEZAJI AGENDA YA 2063 

BOTSWANA

Tanzania imepiga hatua kubwa kwenye utekelezaji wa  makubaliano ya Ajenda 2063, ya kuifanya Afrika kuwa mahali pa ndoto yetu kuelekea Afrika tuitakayo.Chanzo:- Ofisi ya waziri mkuu  kutoka kwenye Mkutano wa kujadili utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa na Wakuu wa Nchi juu ya Ajenda 2063 kwa nchi za Afrika.

Tanzania imepiga hatua kubwa katika utekelezaji wa Ajenda hiyo ikiwemo  masuala ya amani, usalama na demokrasia kupewa kipaumbele kwenye  nchi, kuunganisha miradi mbalimbali ya maendeleo na nchi za Afrika ikiwemo wa SGR,pamoja na miradi ya umeme kupitia nchi za Kenya, Uganda, Ethiopia, na Zambia, na kufungua fursa za kiuchumi kwa nchi za Afrika.

KUMBUKA:- Ajenda ya Afrika 2063 (Afrika tuitakayo) imebeba vipaumbele saba  ambavyo ni kuleta Afrika pamoja kwenye masuala ya Maendeleo,kuunganisha Bara la Afrika kwenye masuala ya kisiasa kwa kutumia tunu za Afrika,Utawala  Bora na unaozingatia sheria, demokrasia,na haki,kuilinda Afrika,Afrika yenye mwelekeo wa utamaduni wake na maadili, Afrika itakayowaletea maendeleo watu wake,kwa manufaa ya wanachi wa Afrika.