SERA ZA FEDHA ZA DKT SAMIA ZAONGEZA MAKUSANYO YA SERIKALI 2023/2024
DARE ES SALAAM
Taarifa kutoka Benki kuu ya Tanzania (BOT) kupitia Kamati yake ya Sera ya Fedha (MPC), inasema katika nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/24 makusanyo ya mapato ya Serikali yamefikia 96% ya lengo la Tanzania Bara huku Zanzibar, makusanyo hayo yakifikia 99.1% ya malengo.
Chanzo:- BOT
Mafanikio hayo yametokana na kuimarika kwa mfumo wa ukusanyaji mapato, usimamizi na utekelezaji wa mikakati ya ulipaji kodi kwa hiari na mapato yanatarajiwa kuongezeka kutokana na hatua zilizochukuliwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan za kuongeza wigo na usimamizi wa kodi.