UPATIKANAJI MAJI SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI WAIMARISHWA
TANZANIA
Serikali katika kuhakikisha inaimarisha miundombinu ya maji shuleni, imefanikisha kufikisha vyanzo vya maji vya uhakika katika shule 5,311 za Sekondari ambapo shule zenye maji ya bomba ni 2,960, visima shule 1,217 na wanaovuna maji ya mvua ni shule 1,134.
Aidha, shule 20,509 za msingi zina vyanzo vya maji ya uhakika ambapo shule zenye maji ya bomba ni 10,965, visima shule 4,966 na shule zinazovuna maji ya mvua ni 4,578.
Vilevile Serikali imetoa maelekezo kwa miradi yote ya ujenzi ya vituo vya afya na ujenzi wa shule mpya ujumuishe miundombinu ya maji inayohusisha kuvuna maji ya mvua, kuunganisha na mifumo ya Mamlaka za Maji na kuchimba visima.