TSH BIL 400 KUWAONGEZEA MAJI SIMIYU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameridhia kiasi cha shilingi bilioni 400 kutekeleza mradi wa kusambaza maji kwa kuhimili mabadiliko ya tabianchi katika mkoa wa Simiyu ambapo umefikia 60% na unatarajiwa kukamilika Desemba 2025 na kuwanufaisha takribani watu 71,726 wanaoishi katika vijiji 18 ndani ya kata saba za Mwamashiga, Mbutu, Isakamaliwa, Kining’inila, Mwamakona, Igurubi na Kinungu.
Mradi huo unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo Awamu ya Kwanza itapeleka maji ya bomba katika miji ya Nyashimo, Bariadi na Lagangabilili pamoja na vijiji vilivyoko umbali wa kilometa 12 kutoka njia kuu za kusambaza maji, huku Awamu ya Pili ikitarajiwa kupeleka maji hayo hadi Mwanhuzi na Maswa.