DKT SAMIA KUZINDUA DARAJA LA KIGONGO -BUSISI MEI 2025
MWANZA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuzindua Daraja la Kigongo Busisi jijini Mwanza mwezi Mei mwaka huu, tayari kwa matumizi ikiwa ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kielelezo na ya kimkakati iliyokamilishwa na Serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Aidha, daraja hilo lenye urefu wa kilometa tatu ni kati ya madaraja makubwa Afrika mashariki na kati na linaunganisha Mkoa wa Mwanza na Geita ambapo linachochea ukuaji wa uchumi kwa wananchi wa Kanda ya Ziwa.