TSH BIL32+ ZAIMARISHA MIUNDOMBINU YA ELIMU DAR
DAR ES SALAAM
Zaidi ya Shilingi bilioni 32 zimetolewa na Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali na ukarabati wa miundombinu ya elimu ya sekondari Jijini Dar es Salaam.
Katika fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni 4.6 kinatumika kwenye ujenzi wa Shule ya Sekondari Kitunda ambako kunajengwa darasa lenye ghorofa na la kisasa, madarasa 16, maktaba ya kisasa, maabara nne na ofisi 12.