TANZANIA, JAPAN KUSHIRIKIANA MIRADI YA AFYA NCHINI

 

TANZANIA, JAPAN KUSHIRIKIANA MIRADI YA AFYA NCHINI

TANZANIA, JAPAN KUSHIRIKIANA MIRADI YA AFYA NCHINI

DODOMA
Tanzania na Japan zimetia saini hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji miradi ya huduma za Afya lengo likiwa kuboresha huduma hizo na kuhuisha ushirikiano kwa kipindi cha miaka mitano (5) kwa kuzingatia vipaumbele vya pamoja.
Utiaji Saini wa makubaliano hayo umefanyika tarehe 8 Januari, 2025 kati ya  Wizara  Afya Tanzania na Balozi wa Japan anayemaliza muda wake Mhe. Yasushi Migawa.
Maeneo ya ushirikiano yatakayofanyiwa kazi ni pamoja na  uboreshaji wa huduma nje ya vituo, rufaa na huduma za kibingwa katika ngazi zote za utoaji huduma za Afya na maeneo mengine ya ushirikiano yakiwa ni uboreshaji huduma za uzazi, afya ya mama na mtoto, kuzuia na kudhibiti magonjwa ya milipuko na matukio mengine ya dharura za Afya.
Aidha Tanzania ipo mbioni kujenga kituo cha umahiri cha usambazaji wa teknoliojia ya tiba ya figo hapa nchini pamoja na nchi jirani, suala ambalo litaijengea Tanzania heshima kubwa katika anga za kimataifa.
Tunapatikana Instagram,Facebook,X, TikTok, YouTube:-BimkubwaTanzania