BARABARA YA NACHINGWEA-RUANGWA-NANGANGA (KM 106) INAJENGWA
LINDI
Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inajenga barabara ya Nachingwea-Ruangwa-Nanganga (KM 106) Mkoani Lindi kupitia Mkandarasi M/s China Railway 15 Bureau Group Cooperation.
Barabara ya Nachingwea-Ruangwa-Nanganga Km 106 ni moja ya Barabara ya kimkakati ambayo katika kuharakisha ujenzi wake imegawanywa sehemu mbili Nachingwea-Ruangwa Km 57.6 na Ruangwa-Nanganga Km 53.2 ambapo kukamilika kwake kutafungua mtandao wa barabara mkoani Lindi na kuchochea uzalishaji wa mazao ya ufuta, mbaazi, korosho na alizeti na hivyo kukuza uchumi wa wananchi wa wilaya za Ruangwa na Nachingwea na kuimarisha sekta ya Usafirishaji na Uchukuzi mkoani Lindi.
Aidha jumla ya wenyeji wa eneo la Ruangwa 165 wamepewa ajira za muda mfupi kutokana na mradi huo na utaratibu huo ni endelevu kadri fursa zinavyojitokeza.
Tunapatikana Instagram,Facebook,X, TikTok, YouTube:-BimkubwaTanzania.
