TSH TRIL 11.5 KWENYE MIRADI KIGOMA

 

TSH TRIL 11.5 KWENYE MIRADI KIGOMA

TSH TRIL 11.5 KWENYE MIRADI KIGOMA

KIGOMA
Takribani sh. Trilioni 11.5 zimetumika katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo
inayoendelea kuunufaisha na kuufungua kiuchumi  Mkoa wa Kigoma katika kipindi cha uongozi wa serikali ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Katika sehemu ya fedha hizo zaidi ya sh.Trilionimoja zinatumika katika ujenzi na upatikanaji waNishati ya umeme kutoka Gridi ya Taifa katika
mkoa huo ambao upo Magharibi ya Tanzaniaukipakana na nchi jirani za Kongo na Burundi.
Serikali inatekeleza miradi mitatu ya umeme katika mkoa wa Kigoma ikiwemo mradi wa uzalishaji wa umeme kutoka mto Malagarasi,
mradi wa njia ya kusafirisha umeme na kituo cha kupokea,kupoza na kusambaza umeme.
Miradi hiyo ya umeme inayotekelezwa katika mkoa huo itakwenda kunufaisha shule za
msingi na Sekondari 983 na maeneo ya kutolea huduma za Afya ya msingi 324 ambayo yamewezeshwa vifaa na vifaa tiba vinayotumia
TEHAMA.