TSH BIL 2.9 KUKARABATI CHUO CHA MAAFISA TABIBU MASWA
SIMIYU
Serikali kupitia Wizara ya Afya, imetenga Shilingi Bilioni 2.9 kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya Chuo cha Maafisa Tabibu kilichopo wilayani Maswa, mkoani Simiyu ujenzi ambao unatarajiwa kukamilika Septemba 2025.
Ukarabati huo unatarajiwa kuimarisha uwezo wa chuo hicho katika kutoa elimu bora na kuongeza mchango wake katika sekta ya afya nchini.
Aidha,chuo kimepanga kuongeza programu mpya katika fani za tiba lishe, mionzi, tabibu meno, na tiba kwa vitendo ikiwa zinalenga kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka 270 wa sasa hadi 960.
