VIJIJI VYOTE 785 MTWARA VYAFIKISHIWA UMEME

 

VIJIJI VYOTE 785 MTWARA VYAFIKISHIWA UMEME

VIJIJI VYOTE 785 MTWARA VYAFIKISHIWA UMEME

MTWARA
Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imefanikiwa kusambaza umeme katika vijiji vyote 785 vya Mtwara, ikiwa ni hatua kubwa ya kuleta mabadiliko vijijini mkoani humo.
Ufikishajii wa umeme katika vijiji vyote mkoani Mtwara umetekelezwa kupitia mradi wa REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili wenye thamani ya shilingi bilioni 71 na tayari umeunganisha vijiji 401 kwenye gridi ya taifa.
Ilani ya uchaguzi ya chama tawala cha CCM ya mwaka 2020-2025 ilielekeza serikali kusambaza umeme katika vijiji vyote nchini ifikapo mwaka 2025.