TSH BIL 450 ZATUMIKA MFUKO WA MAJI

 

TSH BIL 450 ZATUMIKA MFUKO WA MAJI

TSH BIL 450 ZATUMIKA MFUKO WA MAJI

TANZANIA
Serikali kupitia MFUKO wa Taifa wa Maji (NWF) imetumia kiasi cha shilingi bilioni 450 katika kipindi cha uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hasan  kwa ajili ya kufadhili jumla ya miradi 998 ya maji nchini kote kati ya kipindi cha kuanzia Julai 2021 hadi Julai 2024.
Miradi 354 imekamilika na imeanza kutumika na kuwanufaisha Watanzania milioni 5.3 na miradi iliyosalia iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji na mingine inatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka huu wa fedha.
ZINGATIA:- NWF ina jukumu la kutafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji na kutoa mikopo yenye riba nafuu, huku kukiwa na dirisha maalumu la ufadhili wa miradi endelevu ya maji.