TSH BIL 15.7 KULETA MEGAWATI 5,000 JOTOARDHI
TANZANIA
Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa fedha takriban shilingi bilioni 15.7 kwa ajili ya kununua mitambo ya uchorongaji katika maeneo ambayo yameyabainika kuwa na rasilimali ya jotoardhi nchini.
Maeneo yaliyobainishwa kwa ajili ya kupata Nishati ya Jotoardhi ni pamoja na Ruhoi, Natron, Mbozi, Songwe na Kiejo-Mbaka.
Hivi sasa Tanzania inakadiriwa kuwa na vyanzo vyenye uwezo kuzalisha takriban megawati 5,000 na Serikali inayo nia ya kuanza kuzalisha umeme kwa kutumia Jotoardhi.
