TSH 23+ KUSAMBAZA UMEME K’MANJARO VIJIJINI
KILIMANJARO
Zaidi ya shilingi Bilioni 23 zimetumika Kusambaza Umeme Kilimanjaro Vijijini ambapo jumla ya Vijiji 506 Vimeunganishwa Kati ya Vijiji 519 Sawa Na 97.49% huku serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ikjipanga kuhakikisha ifikapo Desemba 2024 vijiji vyote 519 Mkoani Kilimanjaro viwe vimeunganishwa na umeme.
Mkoa wa Kilimanjaro REA inatekeleza jumla ya miradi mikubwa mitatu ambayo ni mradi wa kusambaza umeme vijijini, mradi wa kusambaza umeme kwenye migodi midogo na maeneo ya kilimo na mradi wa kusambaza umeme katika vituo vya afya na visima vya maji.
SOMA HAPA:- Sekta ya umeme ni injini ya uchumi wa taifa lolote duniani na kwakutambua hilo, Mhe Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewekeza fedha nyingi katika Sekta na nishati.