MHE. RAIS DKT SAMIA AONGEZA MUDA WA UOKOAJI KARIAKOO

 

MHE. RAIS DKT SAMIA AONGEZA MUDA WA UOKOAJI KARIAKOO

MHE. RAIS DKT SAMIA AONGEZA MUDA WA UOKOAJI KARIAKOO

BRAZIL
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amemuelekeza waziri mkuu Mhe Kassim Majaliwa  kuongeza muda wa uokoaji katike jengo la ghorofa lililoporomoka eneo la kariakoo Novemba 16, 2024.
Akizungumza kwa njia ya simu Mhe Rais Samia amesema
“Mhe waziri mkuu ninatambua utaratibu wa uokoaji una muda maalumu wa saa 72 mpaka kusitisha zoezi hilo. Binafsi nina matumaini kuwa MwenyeziMungu anaweza akatenda miujiza yake na kuweza kuwanusuru ndugu zetu wengine ambao bado wamenasa kwenye jengo hilo. Ninakupa maelekezo ya kutositisha zoezi la uokoaji na kuongeza muda wa saa 24 zaidi ili kuwapambania ndugu zetu ambao tunaamini bado wako hai”
Aidha Mhe Rais Samia ameongeza “kwa vikosi vyetu vyote na wananchi wote wanaopambana kuokoa maisha ya ndugu zetu katika zoezi hilo ninaomba ufikishe salamu zangu na uwaeleze kuwa natambua na ninawathamini sana. Wameonesha utu,uzalendo mkubwa na uchapakazi wa hali ya juu sana. Hivyo nawatia moyo na kuwapa nguvu ya kuendelea kuwapambania ndugu nzetu kwani ninyi ni mashujaa wa taifa letu”.
Vilevile Mhe Rais Dkt Samia anawaombea kwa Mungu awalinde na kuwapa nguvu muda wote  wakiwa wanatekeleza jukumu hilo kubwa na la kizalendo.
Halikadhalika Mhe Rais  amewasihi wananchi, ndugu na jamaa kuendelea kuwa na subira na kama taifa tuendelee kuwaombea ndugu zetu  na wapiganaji wetu ili tufanikishe zoezi hili kwa mafanikio makubwa.
Mwenyezi Mungu tunakuomba utufanyie wepesi kwenye zoezi hili, Amin.