NCHI 13 ZAKUTANA ARUSHA KUJADILI NISHATI

 

NCHI 13 ZAKUTANA ARUSHA KUJADILI NISHATI

NCHI 13 ZAKUTANA ARUSHA KUJADILI NISHATI

ARUSHA
Wataalamu wa nishati ya umeme kutoka nchi 13 za Ukanda wa Afrika ikiwemo Misri, Rwanda, Congo, Burundi, Kenya, Ethiopia, Malawi,Sudan Kusini, Somalia, Uganda, Djubout na Tanzania wamekutana jijini Arusha (kwa wiki mbili kuanzia Septemba 10) kwa lengo la kujadili  mahitaji ya umeme katika kipindi cha miaka 50 ijayo na namna ya kuvitumia vyanzo vipya vya nishati hiyo ili  kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Wataalam hao kutoka nchi  wanachama wa Easterm Africa Power Pool (EAPP) watajadili namna ya upatikanaji wa nishati ya umeme kupitia vyanzo mbalimbali vya asili ikiwemo joto la Ardhi.
Akizungumza  Katibu mkuu  wa shirika la EAPP,James Wahogo amesema nchi wanachama wa EAPP zinauzalishaji Mkubwa wa umeme na wataangalia namna ya nchi hizo ziweze kupeana umeme kwa kuuziana.
“Tanzania imepiga hatua kubwa katika suala la uzalishaji wa nishati ya umeme kutoka vyanzo asili ikiwemo Gesi na tunaimani katika kipindi cha mbeleni itakuwa na umeme mwingi wa ziada na kuziuzia nchi za jirani”amesema Wahogo.
Aidha Wahogo amezitaja nchi hizo zinazounda umoja wa EAPP kuwa ni Burundi,Comoro, DRC Congo,Djibouti, Misri,Eritrea,Ethiopia, Kenya,Libya, Madagascar, Malawi,Rwanda,Shelisheli,Sudan Kusini ,Sudan,Tanzania, Uganda na Zambia.