KUZINDULIWA KWA SGR, TANZANIA IMETHUBUTU,SAMIA AMEWEZA
DAR ES SALAAM
Historia imeandikwa Agosti mosi 2024 kupitia tukio la Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kufanya uzinduzi wa Reli ya SGR, tukio hili ni uthibitisho kwamba Tanzania imethubutu na Rais Dkt Samia ameweza.
TAARIFA ZA KUSISIMUA KUHUSU SGR
Reli ya SGR imeonesha mfano kwa nchi za Afrika kujenga miundombinu ya Reli ya SGR pasipo kutegemea nchi nyingine (Mikopo/msaada)
Mradi huu wa SGR ya Tanzania ulisanifiwa na kujengwa (designed & built) kwa viwango vya juu zaidi (kwa maana ya uwezo wa kuhimili mizigo inayopitishwa kwenye reli (Axle load of rolling stock).
Wakati reli za SGR zilizojengwa katika nchi zote za Afrika uwezo wake ni Axle load kati ya tani 21-23; wakati SGR ya Tanzania Axle load yake ni tani 35 (yaani ina uwezo wa kubeba mizigo mizito zaidi)
Maendeleo haya yanalenga kuimarisha muunganisho, kukuza ukuaji wa kikanda na kuweka kielelezo kwa miradi ya baadaye ya miundombinu, ikisisitiza umuhimu wa suluhu za kisasa za usafiri katika kuendeleza maendeleo ya kitaifa.
