SERIKALI IMEIMAIRISHA MIUNDOMBINU MOROGORO
MOROGORO
Serikali ya awamu ya sita inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya Kitaifa Mkoani Morogoro ikiwemo Ujenzi wa Barabara ya Mikumi - Kidatu – Ifakara (sehemu ya Kidatu – Ifakara, (km 66.9) kwa kiwango cha lami pamoja na ujenzi wa Daraja la Ruaha Mkuu ambao umefikia asilimia 86% za utekelezaji na tayari Mkandarasi amekamilisha km 55.67 za lami kati ya km 66.9 zinazotakiwa kwa mujibu wa Mkataba.
Pia inaendelea na Ujenzi wa barabara ya Dumila – Kilosa – Mikumi (km 142) kwa kiwango cha lami (sehemu ya Rudewa – Kilosa km 24) kwa kutumia fedha za ndani; Mkandarasi amekamilisha ujenzi wa kilometa 22.05; barabara imekabidhiwa na inatumika, Mkandarasi amekamilisha pia madaraja matatu ya Kobe, Wailonga na Mazinyungu na kwasasa anaendelea na kazi ya km 0.75 ya maungio ya madaraja hayo.
#HodiMorogoroTwakusaaho
