TANI 38.9 MBEGU ZA MALISHO ZASAMBAZWA

 

TANI 38.9 MBEGU ZA MALISHO ZASAMBAZWA

TANI 38.9 MBEGU ZA MALISHO ZASAMBAZWA

TANZANIA
Katika kuimarisha upatikanaji wa malisho hapa nchini, jumla ya tani 38.9 za mbegu za malisho aina ya Napier iliyoboreshwa (Juncao) zimenunuliwa na kusambazwa katika maeneo ya Msomera tani 5, Kongwa Ranchi tani 20, Ruvu Ranchi tani 3.9, na tani 10 katika mikoa ya Morogoro, Pwani na Tanga. 
Aidha, serikali inaendelea kutekeleza mpango wa mashamba darasa ya malisho 150 yenye ukubwa wa ekari 865 katika Halmashauri 71 ambapo jumla ya tani 5 za mbegu za nyasi aina ya Rhodes zimesambazwa katika Mikoa ya Morogoro , Dodoma, Iringa, Rukwa, Katavi, Kigoma, Kagera Geita, Shinyanga, Simiyu, Singida Pwani, Arusha, Manyara, Songwe, Ruvuma na Lindi.