TANI 475,579 ZA SAMAKI HULETA TSH TRIL 3.4

 

TANI 475,579 ZA SAMAKI HULETA TSH TRIL 3.4

TANI 475,579 ZA SAMAKI HULETA TSH TRIL 3.4

DAR ES SALAAM
Takwimu kuhusu masuala ya uvuvi zinaonesha Tanzania inazalisha wastani wa tani 475,579 za samaki wanaojumuisha takribani tani 429,168 za samaki wanaotoka kwenye maji asilia, na kuchangia takribani shilingi trilioni  3.4,  takribani  1.9% ya mchango wa kila mwaka wa sekta katika pato la taifa - (GDP)
Takwimu hii imetolewa na ofisi ya Naibu waziri mkuu na wizara ya nishati katika Mkutano wa Kwanza wa Wavuvi Wadogo Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam uliokwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 10 ya mafanikio katika sekta ya uvuvi.
Aidha wizara ya uvuvi imesema Lengo la mkutano huo ni kuwapa wavuvi wadogo ambao wanafikia 95% ya shughuli zote za uvuvi jukwaa la kueleza mahitaji yao na kuboresha sekta hiyo, kuhakikisha wanashirikishwa katika utungaji wa sera, mifumo ya sheria na mipango mkakati.
Mkutano huo wa wavuvi wadogo ni wa kwanza kufanyika  Barani Afrika (Tanzania), baada ya kuanzishwa na kuadhimishwa  mwaka wa Kimataifa wa Uvuvi na Kilimo cha Majini (IYAFA) jijini Roma, Italia, Machi 2023.