TATOA WAMPONGEZA DKT SAMIA KUVUTIA UWEKEZAJI

 

TATOA WAMPONGEZA DKT SAMIA KUVUTIA UWEKEZAJI

TATOA WAMPONGEZA DKT SAMIA KUVUTIA UWEKEZAJI

DAR ES SALAAM
Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) kimepongeza jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan za kuvutia uwekezaji zaidi nchini.
Pongezi hizo zimetolewa na TATOA wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka mitano ya kampuni ya Xerin Logistics Limited na chakula cha jioni cha iftar iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambayo iliwakutanisha watu mbalimbali wakiwemo watoto yatima na watu wenye ulemavu
Akizungumza kwenye hafla hiyo mwenyekiti wa TATOA Elias Lukumay amesema  “Sekta ya uwekezaji imeimarika katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, jambo ambalo limevutia uwekezaji wa ndani na nje ya nchi, chini ya uongozi wa Rais Samia, serikali imepiga hatua kubwa katika kuhakikisha uwekezaji nchini unakua na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa nchi,katika kipindi cha uongozi wake vijana kadhaa waliwekeza katika sekta mbalimbali zikiwemo biashara za usafirishaji nchini.Amesema Lukumay
Kwa mujibu wa Taarifa ya Uwekezaji wa Kila Robo ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ya Oktoba - Desemba 2023, Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Nje (FDIs) ulichangia asilimia 50.34 ya jumla ya uwekezaji ulioidhinishwa au dola za Marekani milioni 703.00.
Kwa kulinganisha, Uwekezaji wa Ndani (DI) umechukua 49.65% ya jumla ya uwekezaji ulioidhinishwa, ambapo DI ilipata ongezeko kubwa la karibu 201% kutoka robo ya pili mwaka 2022 hadi robo ya pili mwaka 2023.