MWAKA 2023 WAGONJWA MIL 29+ WALIHUDUMIWA
TANZANIA
Mwaka 2023 jumla ya wagonjwa 29,479,636 walihudumiwa katika vituo vya afya ya msingi nchini kote.
Wagonjwa milioni 26.9 walipatiwa huduma katika vituo vya afya ya msingi kama wagonjwa wa nje (OPD) na wagonjwa 854,318 walipatiwa huduma ya kulazwa (IPD). Katika eneo la mama na mtoto jumla ya akina mama milioni 1.6 walijifungua katika vituo vya kutolea huduma ya afya ya msingi na akina mama 125,318 waliokuwa na uzazi pingamizi walifanyiwa upasuaji, hivyo kwa mgawanyo huo unafikisha idadi ya wagonjwa 29,479,636 waliopatiwa huduma katika maeneo tajwa.
