JUMLA YA WALIMU 29,879 WAAJIRIWA
DAR ES SALAAM.
Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Dkt Samia Suluhu Hassan imeajiri jumla ya Walimu 29,879 wa Shule za Msingi na Sekondari za Serikali kati ya Juni, 2021 na Februari 2024.
Walimu hao wamepangiwa shule katika maeneo mbalimbali nchini ili kuongeza nguvu ya utoaji wa elimu , hii ni kutokana na ongezeko la wanafunzi.