ELIMU BILA ADA YAONGEZA WANAFUNZI KWA 152.74%
TANZANIA
Mpango wa Elimumsingi Bila Ada kwa shule za msingi na sekondari nchini umeleta mafanikio makubwa, ikiwa ni pamoja na ongezeko la wanafunzi wapya wanaoandikishwa kujiunga katika ngazi mbalimbali za elimu.
Idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza imeongezeka kutoka wanafunzi 425,743 mwaka 2016 Mpango wa Elimumsingi bila Ada ulipoanza hadi wanafunzi 1,076,037 mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 152.74.
