TSH BIL 916+ KWENYE AFYA MSINGI & VIFAA TIBA
DAR ES SALAAM
Serikali katika awamu ya sita imeendelea kufanya maboresho katika eneo la ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma za Afya ya Msingi na ununuzi wa Vifaa Tiba.
Katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita jumla ya shilingi bilioni 916.6 zimetolewa ambapo kati ya hizo Shilingi bilioni 624,888 ni kwa ajili ya miradi mbalimbali ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kutolea huduma za Afya ya Msingi, Shilingi bilioni 287.5 kwa ajili ya ununuzi wa Vifaa na Vifaa Tiba na Shilingi bilioni 4.21 zilitolewa kwa ajili ya kuendesha mafunzo mbalimbali kwa watoa huduma ikiwemo mafunzo kwa wataalam wa kutoa huduma ya ganzi na usingizi na mafunzo kwa wataalam wanaotoa huduma kwa wagonjwa mahututi na Wagonjwa wa dharura.
