TSH MIL 780 KUNUFAISHA WANANCHI 2,250 MPANDA

 

TSH MIL 780 KUNUFAISHA WANANCHI 2,250 MPANDA

TSH MIL 780 KUNUFAISHA WANANCHI 2,250 MPANDA

KATAVI
Zaidi ya wakazi 2,25O katika vijiji viwili vya Tambazi A na Tambazi B Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi wanatarajia kumalizika kwa kero ya maji baada ya kukamilika kwa mradi wa maji wa wenye thamani ya shilingi milioni 780.
Mradi huo unatekelezwa na  serikali ya awamu ya sita kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Vijijini na Mijini (RUWASA) ikiwa ni juhudi za serikali kuboresha huduma ya maji katika eneo hilo.
Hadi sasa mradi umefikia 80% na unahusisha ujenzi wa tanki la maji lenye uwezo wa kubeba lita 100,000 za kimiminika hicho cha thamani.