TSH BIL 298 ZAJENGA KIWANDA CHA MELI
KIGOMA
Serikali Kupitia Wizara ya Uchukuzi, imeanza ujenzi wa Kiwanda cha kwanza cha kutengeneza Meli Nchini (karakana) ya kudumu katika Ziwa Tanganyika pia itajengwa chererezo yenye uwezo wa kubeba Meli ya uzito wa Tani 5000 ambacho gharama ya kiwanda ni shilingi bilioni 298,mradi huo unaambatana na ujenzi wa Meli mbili za Mizigo katika ziwa Tanganyika na Victoria na huku utekelezaji wa miradi ikigharimu zaidi ya Bilioni 630
(sh bilioni 298 ujenzi wa kiwanda cha meli, na bilioni 332 ujenzi wa meli mbili).
Mkataba wa ujenzi huo wa kiwanda cha meli umesainiwa Oktoba 11, 2023 na utekelezaji wake unafanyika kwa muda wa miaka miwili tangu siku uliposainiwa.
Ujenzi wa Miradi hiyo unatazamwa kuwa hatua Muhimu ya kuinua uchumi wa Mkoa wa Kigoma na Taifa kupitia mzunguko wa biashara kwa nchi za Maziwa Makuu
