SUKARI KUAGIZWA KUTOKA NJE KUPITIA NFRA, CPB
KAGERA
MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), Prof Kenneth Bengesi amesema Serikali inatarajia kuagiza sukari kutoka nje kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) na Bodi ya Nafaka na Mazao Mengine Tanzania (CPB) ili kukidhi viwango vya juu vilivyopo hivi sasa vya mahitaji ya sukari nchini.
Akizungumza mara baada ya kukagua maghala ya sukari na kutathmini taratibu za usambazaji katika maeneo mbalimbali nchini Bwana Bengesi amesema “serikali itafuata taratibu zote za kisheria ili kuhakikisha hakuna ukiritimba katika biashara ya sukari,Wazalishaji wote wa sukari ambao wameruhusiwa kuagiza sukari kutoka nje lazima wahakikishe wanatumia manunuzi kwa wingi ili waweze kuagiza kiasi cha kutosha,"
Aidha Mkurugenzi wa SBT amewaonya waagizaji na wafanyabiashara wa sukari ambao bado wanauza sukari hiyo kwa bei ya juu kinyume na maagizo ya serikali.
"Serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria na kinidhamu kwa wale ambao watabainika kuuza sukari kwa bei ya juu," amesema
