TAZAMA MAKALA HII KUPITIA:https://www.youtube.com/watch?v=7NN27jCqfGk
PATO LA TAIFA KUONGEZEKA MWAKA 2024
Ripoti ya sera ya fedha iliyotolewa hivi punde na BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) inasema uchumi wa Tanzania unatarajiwa kukua hadi kufikia asilimia 5.5 mwaka huu, kutokana na uwekezaji katika miundombinu,uwekezaji wa kwenye sekta za umma na binafsi, mageuzi ya kuboresha hali ya biashara, hali ya hewa nzuri, ukuaji katika sekta ya utalii, na sera za serikali ya awamu ya sita zinazounga mkono biashara.
