TANZANIA, INDONESIA ZASAINI MoU’S KUKUZA BIASHARA, UWEKEZAJI

 

TANZANIA, INDONESIA ZASAINI  MoU’S  KUKUZA BIASHARA, UWEKEZAJI

TANZANIA, INDONESIA ZASAINI  MoU’S  KUKUZA BIASHARA, UWEKEZAJI

INDONESIA

Tanzania na Indonesia zimetia saini hati nne za Makubaliano (MoU’s) mapema (Leo) Januari 25 zenye kuweka nia njema ya mshikamano mkubwa wa kibiashara.

Mikataba hiyo imesainiwa mbele ya Rais wa Tanzania Dkt  Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Rais wa Indonesia, Joko Widodo.Makubaliano yaliyotiwa saini yamelenga ushirikiano wa kujenga uwezo wa kidiplomasia, kilimo, madini na uchumi wa bluu.

Akizungumza mara baada ya utiaji saini huo, Rais Samia amesema wakati nchi hizo zikishiriki maono ya kukuza uwekezaji baina yao pia ameahidi kushiriki katika kongamano lijalo la biashara na uwekezaji kati ya Indonesia na Tanzania.

Aidha Dkt amesema"Rai yangu kwa washirika wa sekta binafsi ni kwamba, wakati mzuri wa kuwekeza Tanzania ni miaka miwili iliyopita lakini wakati wa pili bora ni sasa," Rais Samia amebainisha.

Aidha Mhe Samia ameongeza "Katika uhifadhi wa kimataifa juu ya kulinda mazingira yetu Tanzania inaendelea kutilia mkazo upatikanaji wa nishati na teknolojia safi na salama za kupikia...tulikubali kufanya kazi kwa karibu zaidi na kubadilishana uzoefu na Indonesia katika kuunga mkono ufumbuzi wa kupikia safi barani Afrika," 

Ziara ya Rais  Dkt Samia nchini Indonesia inakuwa ziara yake ya kwanza ya kikazi ya kimataifa kwa mwaka 2024.

#BIMKUBWAINDONESIA