SGR KUSAFIRISHA MIZIGO MAPEMA 2025
ZANZIBAR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amesema reli ya kisasa nchini (Standard Gauge Railway – SGR) inatarajiwa kuanza kusafirisha mizigo mapema 2025 kutoka Dar es salaam hadi Dodoma.
Mhe.Dkt Samia ametoa kauli hiyo leo (jumanne) Desemba 31 ,2024 wakati akilihutubia Taifa kutoka Ikulu ndogo ya Tunguu Zanzibar ikiwa ni hotuba ya mwisho wa mwaka 2024.
Katika hatua nyingine Mhe Rais Samia amesema serikali itanunua mabehewa ya abiria na mizigo kwa ajili ya kipande cha reli kutoka Mwanza hadi Isaka
KUMBUKA:- SERIKALI KUPITIA SHIRIKA LA RELI TANZANIA (TRC) IMEPOKEA MABEHEWA 264,KATIKA MABEHEWA HAYO 200 NI YA KUBEBA MAKASHA (MAKONTENA) NA MABEHEWA 64 NI YA KUBEBA MIZIGO ISIYOFUNGWA (LOOSE CARGOES). SHEHENA HIYO YA MABEHEWA 264 NI SEHEMU YA JUMLA YA MABEHEWA 1,430 AMBAYO KWA MUJIBU WA MKATABA YANATENGENEZWA NA KAMPUNI YA CRRC YA NCHINI CHINA
