UWEPO WA  SGR WAINGIZA TSH BIL 358.74

 

UWEPO WA  SGR WAINGIZA TSH BIL 358.74

UWEPO WA  SGR WAINGIZA TSH BIL 358.74

DODOMA
 Tangu kuanzishwa kwa mradi wa usafiri wa reli ya kisasa (SGR) serikali imezalisha ajira za watu zaidi ya 30,176 za moja kwa moja na 150,000 zisizo za moja kwa moja ambapo ongezeko hili la ajira limechangia serikali kuingiza mapato ya shilingi bilioni 358.74.( Hii ni kwa mujibu wa ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji). 
Fursa zingine ambazo zimepatikana ni viwanda, wazabuni na wakandarasi ambapo hadi sasa jumla ya makampuni 2,460 yanashiriki katika mradi huo wenye thamani ya shilingi trilioni 3.69.
Mradi wa SGR unaendelea kuchochea kwa kasi ongezeko la mahitaji ya saruji na vifaa vya ujenzi na kuifanya sekta ya viwanda kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi
Aidha tangu kuanza kwa safari za (SGR) abiria waliosafiri  ni 645,421 ambapo serikali imeingiza shilingi bilioni 15.695. 
MUHIMU:- Mradi wa usafiri wa reli ya kisasa (SGR) umeweza kuongeza kipato cha serikali kutokana na ongezeko kubwa la abiria Na kuongeza tija katika shughuli za utalii hasa katika maeneo yanayopita ikiwemo Hifadhi ya Mikumi na Hifadhi ya Ruaha (kupitia Stesheni ya Kilosa), Hifadhi ya Katavi (Stesheni ya Tabora), Hifadhi ya Gombe (Stesheni ya Kigoma), na Hifadhi ya Serengeri (kupitia Stesheni za Malampaka na Mwanza).