MRADI WA BONDE LA MSIMBAZI MBIONI KUTEKELEZWA
DAR ES SALAAM
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam (DCC) imefungua zabuni ya ujenzi wa matuta na ulinzi wa kingo za mto katika Bonde la Msimbazi chini, ikiwa ni sehemu ya Mradi wa Maendeleo ya Bonde la Msimbazi (MBDP).
Mradi huu unatekelezwa na serikali kwa kufadhiliwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Kimataifa (IDA) kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 200 (zaidi yash bilioni 466), ambapo mradi huu unalenga kupunguza hatari za mafuriko na kufufua eneo la mto kwa ajili ya maendeleo ya mijini na matumizi ya mengine.
Pamoja na msaada wa IDA mradi huo unafadhiliwa kwa pamoja kupitia mkopo wa dola za Marekani milioni 30 (karibia shilingi bilioni 70) kutoka Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Uhispania na ruzuku ya Euro milioni 30 (shilingi bil 69.4) kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Uholanzi.
DCC kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), na Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), imetangaza kuanza kwa kazi muhimu za ujenzi zitakazotatua kero za muda mrefu za mafuriko katika meneo ya mkoa wa Dar es Salaam yaliyo hatarini zaidi
Upeo wa mradi ni pamoja na uundaji wa tambarare za mafuriko, kuongeza kina na kupanua njia za mito na kujenga matuta ambayo yanaweza kuchukua maendeleo ya miji ya baadaye na maeneo ya umma.
Mara tu Bonde la Msimbazi litakapokamilika, litakuwa na uwezo wa kusaidia maeneo ya burudani, maeneo ya kijani kibichi na upanuzi wa miji salama, na hivyo kuchangia ukuaji wa jumla wa jiji la Dar es Salaam na kisasa.
Aidha mradi huo ni sehemu ya jitihada zinazoendelea za kuboresha miundombinu ya jiji la Dar es Salaam na kukabiliana na changamoto zinazoletwa na ongezeko la ukuaji wa miji na mafuriko yanayotokana na mabadiliko ya tabianchi.
Mradi umepangwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi 24, na awamu ya awali ya miezi miwili ya uhamasishaji.
