SERIKALI YAWAGUSA WANA MPITIMBI KWA HOSPITALI

 

SERIKALI YAWAGUSA WANA MPITIMBI  KWA HOSPITALI

SERIKALI YAWAGUSA WANA MPITIMBI  KWA HOSPITALI

RUVUMA
Serikali imewaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya wananchi wa Kata ya Mpitimbi Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma baada ya kuboresha huduma za afya katika hospitali ya Halmashauri hiyo iliyojengwa Kijiji cha Mpitimbi Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma.
Hospitali ya Mpitimbi inatoa huduma kwa wananchi wa nchi Jirani ya Msumbiji ambao wanapakana na Jimbo la Peramiho katika Kijiji cha Mkenda kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
Aidha hapo awali wananchi wa Kata ya Mpitimbi na Tarafa ya Muhukuru matibabu yao ya kibingwa ilikuwa ni lazima wayapate kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa,Songea au Kwenda kwenye hospitali ya Rufaa ya Misheni ya Mtakatifu Joseph Peramiho.